Thursday, May 15, 2014

AJIRA ZETU MBEYA NI NINI?

Mtandao huu wa AJIRA ZETU MBEYA unamilikiwa na kampuni ya New Position Co Ltd.
Kampuni ya NEW POSITION ni kampuni iliyosajiliwa kisheria chini ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa namba 105407 yenye lengo la kuwaunganisha waajiri na waajiri popote nchini Tanzania.
Kampuni hiyo ni wakala wa ajira na kazi ambayo kazi yake ni kuwatafutia ajira wahitimu wa ngazi mbali mbali wanaohangaika kuomba kazi katika mashirika mbali mbali ikiwa ni pamoja na mashirika au makampuni yanayohitaji wafanyakazi.
Kampuni hii kwa sasa inafanya kazi zake mkoani mbeya na maeneo ya jirani.
Kampuni ya NEW POSITION pia inaubia na kampuni ya BOLSTO inayohusika na uuzaji wa mashine mbali mbali za Kielectroniki kama vile EFDs ambazo ziko za aina tofauti tofauti  ambazo ni Prima, Dp25, Best LC, Ultima na Easy Machines inayofanya kazi ya uwakala wa fedha kama Mpesa, Tigo Pesa, Zuku, Dstv nk.



Unawezaje kufaidika na mtandao wa AJIRA ZETU MBEYA?
Kupitia mtandao huu kuna faida nyingi sana unazoweza kuzipata. Baadhi ya faida hizo ni;
1. Kama wewe ni mwajiri au unatafuta mfanyakazi kupitia mtandao huu na kampuni ya NEW POSITIO utaweza kukutanishwa na mtu anayekufaa kulingana na mahitaji yako.
2. Kama unatafuta ajira utapata matangazo mbalimbali ya nafasi za ajira. Pia utaunganishwa na waajiri na kuweza kupatiwa kazi kulingana na sifa zako.
3. Kama unatafuta ajira kwa muda mrefu na hupati huenda kuna mbinu nzuri hujazijua za kuandika wasifu wako ili kuweza kuwashawishi waajiri. Kupitia kampuni ya NEW POSITION utaweza kufundishwa mbinu bora za kuandika wasifu utakaoshawishi mwajiri akuajiri.
4. Kupitia mtandao huu utajifunza jinsi ya kujibu maswali ya usaili wa nafasi za kazi.
5. Utapata taarifa mbalimbali za kazi na biashara kupitia matangazo.
Karibu sana kwenye mtandao wako wa AJIRA ZETU MBEYA ili uweze kufurahia maisha yako ya ajira.





0 comments:

Post a Comment